Kansela Merkel na waandishi habari wakosoaji China | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kansela Merkel na waandishi habari wakosoaji China

Si miko kuzungumzia demokrasia hata katika jamhuri ya umma wa China

Kansela Merkel azungumza na wanafunzi mjini Beijing

Kansela Merkel azungumza na wanafunzi mjini Beijing

Kansela Angela Merkel akiendelea na ziara yake katika jamhuri ya umma wa China,hii leo amekutana na waandishi habari wanaokosoa sera za nchi hiyo.Wanasayansi na wana mtandao ni miongoni mwa walioshiriki mazungumzoni.

Miadi yao ilipangwa kua baada ya chai ya asubuhi.Saa mbili na dakika 45 kansela Angela Merkel akakutana na kundi dogo la waandishi habari wakosoaji wa kichina.Mwaka mmoja kabla ya michezo ya Olympics,waandishi habari wanajikuta wanazidi kukandamizwa na kubughudhiwa katika jamhuri ya umma wa China.Visa hivyo vinaanzia kusikilizwa yote wanayosema,kuwekwa katika vifungo vya nyumbani hadi kufikia korokoroni.Neno uhuru wa vyombo vya habari ni geni nchini China.

Kwa kukutana na waandishi hao wa habari,kansela Angela Merkel amedhihirisha,anataka kuzungumzia misingi ya kidemokrasi sio tuu pamoja na viongozi wa kisiasa wa China,bali pia na wale wanaoathirika moja kwa moja na visa vya ukandamizaji.

Li Datong mmojawapo wa walioshiriki mazungumzoni anasema tunanukuu:

„Kansela alitaka kujua hali namna ilivyo katika vyombo vya habari vya China.Alitaka aarifiwe yanayotokea,alitaka kujua hali namna ilivyo nchini China pamoja na hamu iliyoenea katika jamii.“

Hivyo ndivyo Li Datong anavyotathmini mazungumzo yao pamoja na kansela.Yeye binafsi anasema ameridhika na mazungumzo yao.

„Anapenda kujumuika na watu.Anaonyesha anaijua vizuri hali ya mambo nchini China,hakuhitaji maelezo mengi.Nnahisi kansela huyu wa Ujerumani anapendelea kweli kuona misingi ya kidemokrasi inachipuka,hali ya haki za binaadam inaimarika na uhuru wa mtu kutoa maoni yake unaheshimiwa nchini China.

Li Datong ameshuhudia mwenyewe, bughudha na visa vya ukandamizaji,vinafanana na nini.Alishiriki katika vuguvugu la kudai demokrasia mwaka 1989.Baada ya kuvunjwa nguvu vugu vugu hilo na damu kumwagika,Li alipigwa marufuku kuendelea na shughuli zake kama mwandishi habari kwa muda wa miaka 5,kabla ya kuruhusiwa upya kati kati ya miaka ya 90.

Li alianza kufanya kazi na gazeti la „China Youth Daily“.Alikua akiandika kwa ujasiri ripoti alizozipa jina „kiwango cha kuganda kama barafu.“

Alipogunduliwa anaiwekea suala la kuuliza nadharia ya serikali,akafukuzwa kazini.Tangu wakati huo Li Datong ameorodheshwa kama miongoni mwa wapinzani wakubwa wa serikali.Anasema:

„Kusema kweli,sina nafasi tena ya kuajiriwa.Hawaniachi nifanye kazi,kwa hivyo nnasoma na akuandika.Ripoti zangu zinachapishwa ng’ambo tuu.

 • Tarehe 28.08.2007
 • Mwandishi Aldenrath Petra/ Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CH8z
 • Tarehe 28.08.2007
 • Mwandishi Aldenrath Petra/ Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CH8z

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com