1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel Akamilisha Ziara ya Siku Tatu China

8 Julai 2014

Kansela Angela Merkel amewahutubia wanafunzi mjini Beijing na kutetea faida za "jamii iliyo huru na ya uwazi" akikumbusha maendeleo yaliyotokana na kuporomoka ukuta wa Berlin mwaka 1989.

https://p.dw.com/p/1CY0I
Kansela Angela Merkel akihutubia wanafunzi katika Chuo kikuu Mashuhuri TsinghuaPicha: Reuters

Akiwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu mashuhuri cha Tsinghua,kansela Merkel ameshauri China izidi kuacha wazi masoko yake kwa bidhaa kutoka nje na kupendekeza mageuzi zaidi.Kansela amesema maendeleo yanaimarika watu wanapoyadadisi.Kansela Merkel ametetea maendeleo endelevu,bidii,ulinzi wa mazingira na kuwajibika jamii."Watu wanabidi wahakikishe yote hayo yanafuata mkondo mmoja.Na ndio maana kupungua kiwango cha ukuaji wa kiuchumi ni suala la kimantiki.Suala la ukuaji imara wa kiuchumi linazuka pia nchini China.Kwasababu masuala kuhusu usafi wa hali ya hewa na mazingira yanakamata nafasi muhimu.Wale ambao leo hii wanaishi vizuri na kula vizuri,wanataka kujua kuhusu ubora wa hayo."

Maendeleo imara ya nchi yanahitaji sio tu teknolojia na shughuli za kiuchumi bali pia mfumo wa haki wa sheria na ulio sawa kwa wote katika jamii."Ni muhimu raia wanapokuwa na imani na mfumo wao wa sheria" amesema kansela Angela Merkel kabla ya kuzungumzia kongamano ambalo China na Ujerumani wanazungumzia kuhusu masuala ya haki za binaadam,uhuru wa kila raia na jamii ya mchanganyiko wa makabila tofauti.

Majadiliano ni muhimu pia akwa China

"Ni muhimu kupita kiasi ,kwasababu mapinduzi ya amani yalipotokea miaka 25 iliyopita katika ile iliyokuwa ikijulikana kama jamhuri ya kidemokrasia ya Ujerumani,ukuta wa Berlin uliporomoka na majadiliano huru kuanza-ameelezea kansela Angela Merkel na kukumbusha yeye binafsi amekulia katika ile iliyokuwa ikijulikana wakati ule kuwa ni kambi ya Usovieti ambako uhuru ulikuwa ukikandamizwa na wananchi kuchunguzwa."Nnahisi ni muhimu majadiliano kama hayo kuanzishwa pia nchini China" amesisitiza.

Angela Merkel Peking China 8.7.2014
Kansela Merkel baada ya hotuba yake huko TsinghuaPicha: Reuters

Wanafunzi katika ukumbi huo waliduwaa kusikia matamshi hayo ya kansela.Mwanafunzi wa fani ya kiufundi Zhang Cong alinong'ona "matamshi bayana kama haya ndio tunayoyahitaji.

Mikataba kadhaa imetiwa saini

Mbali na hotuba hiyo mbele ya wanafunzi katika chuo kikuu cha Tsinghua,ziara ya siku tatu ya kansela Merkel nchini China imepelekesa kutiwa saini mikataba kadhaa ya akibiashara na uwekezaji.Kampuni la magari la Ujerumani Volkswagen limepatiwa kibali cha kufungua matawi mawili ziada nchini China na kampuni la Airbus limeagiziwa helikopta zaidi ya 100 na China.

Angela Merkel China 7.7.2014
Kansela Merkel akaizungumza na ujumbe aliofuatana nao kaatika mkutano wa pande mbiliPicha: Reuters

Kansela Angela Merkel na mwenyeji wake Li Keqiang wamesisitiza nchi zao zinataka kuimarisha ushirikiano kati yao.China itakuwa mshirika wa maonyesho ya kimataifa ya computa Cebit 2015 mjini Hannova mwakani.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman