1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kandarasi za Ulinzi Iraq zaigharimu Marekani mabilioni

P.Martin18 Agosti 2008

Kandarasi za makampuni binafsi huko Iraq na katika nchi jirani,zitaigharimu serikali ya Marekani zaidi ya dola bilioni 100,ifikapo mwisho wa mwaka 2008.

https://p.dw.com/p/F010
*** Philipp, US-Sicherheitsfirma Blackwater - eine "Schattenarmee" der Bush-Regierung? *** ** FILE ** Blackwater USA founder Erik Prince testifies before the House Oversight Committee on Capitol Hill in Washington in this Oct. 2, 2007 file photo. The State Department promised Blackwater USA bodyguards immunity from prosecution in its investigation of last month's deadly shooting of 17 Iraqi civilians, The Associated Press has learned. (AP Photos/Susan Walsh, File)
Erik Prince,Mwenyekiti wa Blackwater.Picha: AP

Wakati huo huo inasemekana kuwa Rais wa Marekani George W. Bush anaeunga mkono kwa dhati utaratibu wa kutoa kandarasi kwa makampuni binafsi,anajiandaa kuyaweka makampuni ya ulinzi kama vile Blackwater chini ya ushawishi wa kisiasa.

Rais Bush licha ya kuunga mkono kile alichokieleza kama dhima muhimu inayobebwa na wakandarasi katika nchi za ngámbo,serikali yake ilishindwa kufikisha mahakamani kwa wakati maelezo ya kuitetea kampuni ya Blackwater.Kwani katika kesi ya Florida,familia za wanajeshi watatu wa Kimarekani waliouawa Afghanistan mwaka 2004 katika ajali ya ndege ya kampuni ya Blackwater Aviation,wameishtaki kampuni hiyo wakitaka kulipwa fidia.Kwa sehemu fulani,kampuni hiyo imeshtakiwa kuambatana na uamuzi wa ripoti za serikali ya Marekani kuwa vifo hivyo vimetokana na makosa yaliyofanywa na wafanyakazi wa Blackwater.

Sasa Blackwater na wale wanaoiunga mkono kampuni hiyo iliyopewa kandarasi ya ulinzi nchini Iraq na Afghanistan,wameingiwa na wasiwasi kwa sababu Washington imebakia kimya.Mawakili wa kampuni hiyo na wakandarasi wengine wanasema,ikiwa kesi ya Florida na zingine zilizofanana zitaruhusiwa kusikilizwa mahakamani,basi huo utakuwa mfano wa hatari.Wao wanahofia kuwa uamuzi wa aina hiyo utasababisha hasara kubwa kwa wakandarasi na utaongeza gharama za bima na hivyo kuathiri vibaya uwezo wao katika utekelezaji wa kazi walizopewa na serikali ya Marekani.

Baadhi ya watazamaji wanadhani kuwa serikali imebakia kimya kuhusu kesi ya Florida,kwa sababu mada ya kandarasi ni suala lililozusha mabishano na mwaka huu nchini Marekani kuna kinaynganyiro cha uchaguzi wa rais.Kesi ya Florida inayoweza hatimae kuishia katika Mahakama Makuu ya Marekani, inauliza iwapo Blackwater na makampuni mengine yaliyopewa kandarasi nchi za ngámbo,yapo chini ya sheria ya Marekani.Suala hilo limezuka kwa sababu ya amri iliyotolewa mwaka 2005 na Mmarekani aliekuwa mwongozi wa Iraq wakati huo.

Kwa upande mwingine,serikali ya Iraq inadai kuwa Blackwater na wakandarasi wengine wanabeba dhamana ya baadhi ya vifo vya raia wa Kiiraqi na inataka sheria ya Iraq itumike kwa wakandarasi hao.Marekani lakini inapinga hatua hiyo.Inadhaniwa kuwa hilo ni miongoni mwa masuala yanayokwamisha majadiliano yake pamoja na Iraq kuhusika na hadhi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq katika zijazo.

Kwa upande mwingine,ripoti mpya iliyotolewa na Ofisi ya Bajeti ya Bunge CBO inasema,hadi hivi sasa,Washington imetumia kati ya dola bilioni 6 hadi bilioni 10 kuwalipa wakandarasi kwa huduma za ulinzi.Inakadiriwa kuwa nchini Iraq makampuni ya ulinzi yana kati ya wafanyakazi 25,000 hadi 30,000.Na kama asilimia 20 ya fedha zinazotolewa kwa operesheni za nchini Iraq huenda kwa wakandarasi.Hivi sasa kuna si chini ya wakandarasi 190,000 nchini Iraq na katika nchi za jirani.Kwa mujibu wa ripoti hiyo Marekani inategemea sana huduma za wakandarasi nchini Iraq kinyume na ilivyokuwa wakati wa vita vyote vingine.

Seneta Kent Conrad wa chama cha Demokrat katika jimbo la North Dakota, ambae pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Bajeti ya Seneti amesema, serikali ya Rais Bush imeweka mfano wa hatari kwa kutegemea hivyo wakandarasi wa kijeshi.Amesema,mtindo huo unazuia uwajibikaji; unakaribisha ulaji rushwa na maovu na wakati mwingine gharama hizo huenda hata zikabebwa na walipa kodi.