1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampuni ya China yakanusha kuhusika na kashfa barani Afrika

22 Novemba 2017

Kampuni moja ya nishati ya China imekanusha kuhusika na kashfa ya ufisadi wa mamilioni ya dola, kwa kujipatia mkataba barani Afrika.

https://p.dw.com/p/2o4Hh
Wahlplakat Cheikh Tidiane Gadio Dakar, Senegal
Picha: DW

Kampuni moja ya nishati ya China imekanusha kuhusika na kashfa ya ufisadi wa mamilioni ya dola, ambayo waendesha mashitaka nchini Marekani wanasema iliratibiwa na wafabiashara wake wawili wa kampuni hiyo kujipatia mkataba barani Afrika.

Taarifa ya hapo jana ya kampuni ya CEFC China Energy inasema kuwa haihusiki na mashitaka ya ufisadi, utakatishaji fedha haramu na kula njama yaliyofunguliwa dhidi ya waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Hong Kong, Patrick Ho na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Senegal, Cheikh Gadio.

Waendesha mashitaka wanasema Gadio na Ho waliratibu rushwa kwa muundo wa michango ili kufaidika kibiashara katika mataifa ya Chad na Uganda kwa ajili ya kampuni moja yenye makao yake mjini Shanghai.

Shirika la habari la Marekani, Associated Press, linasema hati za mahakama za kesi hiyo ya  aina yake zinaibua mikakati mikubwa ya China barani Afrika, ikihusisha pia mafungamano na matukio ya sasa nchini Zimbabwe.