Kampuni la Fiat laimezea mate Opel | Magazetini | DW | 05.05.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Kampuni la Fiat laimezea mate Opel

Jee kunazuka kampuni kubwa kupita yote la kutengeneza magari?

Kitambulisho cha Fiat na Opel

Kitambulisho cha Fiat na Opel

Watoto 23 elfu walipelekwa hospitali nchini Ujerumani mwaka jana kwasababu ya kulewa mpaka kuzimia.Hiyo ndio mada kuu magazetini hii leo.Mada nyengine iliyowashughulisha wahariri wa Ujerumani ni jinsi kampuni la magari la Italy,Fiat linavyoonyesha kuvutiwa na kampuni la magari la Opel.Kuhusu mada hii gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linaandika:

Katika makao makuu ya Opel na katika baraza linalopigania masilahi ya wafanyakazi wa Opel,viongozi wangependelea zaidi kuliona kampuni lao likiungana na Magna.Lakini hawana njia nyengine sasa isipokua kuzingatia kwa dhati mapendekezo ya hivi karibuni ya Fiat.Wanaopaza sauti kudai wateja watoe zaidi na wadhamini mengi zaidi,wanabidi washushe sauti zao.Kwamba serikali kuu inataka ihakikishiwe kikamilifu kabla ya kufikiwa makubaliano,inatosha.Hata kama hofu zinaeleweka,haifai lakini kuwatia kishindo wateja.Hatusemi watu wawapigie magoti na kuwashukuru lakini sauti kali na masharti makubwa makubwa pia hawastahiki tena kutoa wakuu wa Opel."

Hayo ni maoni ya FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG,linalozungumzia pia juu ya kuendelea kuwepo vituo vitatu kati ya vinne vya kuchanganyishia magari nchini Ujerumani.Nalo gazeti la Die Welt lina maoni mengine kabisa na linaandika:

Fiat si mbabe mwenye imani waliokua wakimuota wafanyakazi wa Opel .Mkubwa,tajiri na aliye tayari kuliacha kampuni la Opel liendelee na shughulio zake kama zamani.Na yeye pia anadaiwa nyumbani huko Turin.Lakini Fiat linajivunia kiongozi mwerevu,na mwenye bashasha.Kila kitu kina lingana na,magari madogo maadogo yanaanza upya kupendwa.Nchini Marekani,mpango huu mpya wa Fiat haujawaudhi hata kidogo viongozi wa Chrystler."

Gazeti la SÜDDEUTSCHEN ZEITUNG linasema hakuna chochote cha kuvutia katika mpango wa Fiat.Gazeti linaendelea kuandika:

"Fiat,Chrystler na tawi la Ulaya la General Motors yachanganywe na kuwa kampuni jipya kubwa kabisa la magari .Na kutokana na idadi ya magari yatakayotengenezwa na mauzo yake lifikie kiwango cha kulinganishwa na Volksawagen au Toyota.Lakini Marchionne asijidanganye ,mpango wake hauwezi kufa nikiwa.Meneja huyo wa kitaliana anataka kuyachukua makampuni matatu muflis,kutoka nchi tatu tofauti na zenye mila na desturi tofauti na kuyachanganya.Hakuna hata moja kati ya makampuni hayo,lenye rasli mali seuze teknolojia au mbinu.Si ndio maana yanazongwa na matatizo!

Deutschland Drogenbeauftragte der Bundesregierung Sabine Bätzing

Bibi Sabine Bätzing,mjumbe maalum wa serikali kuu anaepambana na vinywaji vikali na madawa ya kulevya kwa watoto

Hivi sasa tunaiingilia mada yetu ya pili magazetini.Inahusu jinsi baadhi ya watoto wanavyoyatia hatarini maisha yao kwa kutumia vinjwaji vikali vikali vya ulevi.Hayo yametajwa katika ripoti ya mjumbe maalum wa sertikali kuu ya Ujerumani anaepambana na visa vya watoto kutumia vinjwaji vikali na madawa ya kulevya,bibi Sabine Bätzing.Kwa mujibu wa ripoti hiyo,watzoto 23 elfu walilewa mpaka kupoteza fahamu mwaka jana na kupelekwa hospitali.Gazeti la WESTDEUTSCHE ALLGEMEINE ZEITUNG linaandika:

Kama sababu ni matangazo ya biashara ambayo mjumbe huyo maalum wa serikali kuu anataka yapigwe marufuku.Jibu ni ndio.Lakini zaidi anahisi kuna kasoro, nini watoto wafanye wanapokua na wakati wa mapumziko .Badala ya kutoa jasho lao la moyo kwa kufanya spoti au japo kwa kwenda kupoteza wakati katika vituo vya vijana,ambako hakuna mipango ya kuvutia,watoto wanatuliza tafrani zao kwa kunywa biya,mvinyo na vinywaji vyengine vikali.Wizara za familia na serikali za miji zimeshindwa kutia njiani mikakati ya maana kuweza kuwavutia vijana na watoto,wanapokua hawana la kufanya-analalamika mjumbe huyo maalum wa serikali kuu

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul Rahman

 • Tarehe 05.05.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Hk3Y
 • Tarehe 05.05.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Hk3Y