1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za kansela Angela Merkel

Zainab Aziz
8 Septemba 2017

Angela Merkel ndio sura hasa ya chama cha Christian Democratic Union (CDU) na mwaka huu anagombea muhula wa nne wa Ukansela wa Ujerumani. Merkel anakusudia kuiongoza Ujerumani kwa kutumia busara na ubunifu.

https://p.dw.com/p/2jbqS
Deutschland Angela Merkel Wahlkampf in Heidelberg
Picha: picture-alliance/dpa/U. Anspach

Kwa sasa limekuwa ni jambo la kila siku kumuona Angela Merkel akienda kusini, kaskazini , magharibi na mashariki nchini kote Ujerumani katika juhudi za kuendesha kampeni yake ya uchaguzi.  Kansela Merkel hadi kufikia siku ya uchaguzi tarehe 24 Septemba atakuwa amehutubia mikutano zaidi ya hamsini. Hadi sasa maelfu ya wananchi wamekwenda kumsikiliza anapohutubia.  Hata hivyo mara nyingine hutokea watu wachache wenye itikadi za mirengo ya siasa kali wanaojaribu kuvuruga mikutano hiyo. Bibi Angela Merkel mwenye umri wa miaka 63 amezidi kuimarika tangu aingie madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2005. 

Deutschland Wahlkampf CDU- Merkel in Bitterfeld
Wanaompinga kansela Angela Merkel Picha: DW/K.-A. Scholz

Maswala ambayo anayashughulikia ni pamoja na usalama, dhima ya Ujerumani duniani na kuwaingiza wa raia wapya katika jamii.  Kiongozi huyo wa Ujerumani halizungumzii swala la wakimbizi wakati wote, hata hivyo mnamo mwaka 2015 aliruhusu maalfu ya wakimbizi kuingia nchini licha ya sera ya hapo awali ya chama chake cha CDU.  Kwa mujibu wa sera hiyo chama hicho kilitaka wageni waliokuja kufanya kazi wawepo nchini kwa muda tu. Takriban robo ya watu wenye nasaba ya kigeni wanaoishi Ujerumani ni uthibitisho kwamba nchi hii inapendelewa na wageni na kutokana na ukweli huo kansela Angela Merkel alifanya mageuzi ya sera na kuwakubali wahamiaji sera ambayo kwa muda mrefu ilikuwa inatetewa na wapinzani wa vyama vya mrengo wa kushoto. Mwaka huo wa 2015 ulileta neno jipya "Tutaweza” maana yake kuyatatua matatizo.

Jina la Kansela Angela Merkel linaambatanishwa na harakati za kisiasa na katika maswala muhimu. Mengine ni yenye utashi, mfano kuibatilisha sheria ya kulitumikia jeshi kwa lazima, kujiondoa kwenye nishati ya nyuklia na uamuzi wa bunge wa kuridhia ndoa kwa jinsia zote.  Kutokana na maswala hayo Angela Merkel ametoa msimamo na mchango wake katika kuituliza jamii. Licha ya mijadala hiyo maadili ya msingi ya chama cha Christian Democratic Union (CDU) yamebakia pale pale.

Mwandishi: Zainab Aziz/Strack, Christoph

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman