Kampeini za pambamoto siku ya mwisho Marekani | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.11.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Kampeini za pambamoto siku ya mwisho Marekani

Magazeti mengi duniani 'yanamfagilia' Obama

Kiongozi wa Venezuela, Hugo Chavez, nae amtakia ushindi Obama

Kiongozi wa Venezuela, Hugo Chavez, nae amtakia ushindi Obama

Siku ya mwisho ya kufanya kapeini kwa wanaotaka kwenda Ikulu nchini Marekani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni leo jumatatu.

Wagombea wawili wa kiti hicho.Maseneta Barack Obama wa chama cha Democratic na mpinzani wake John McCain wa Republican wanaendesha kampeini kali siku za mwisho hasa katika majimbo saba kuweza kuwashawishi wale ambao baado hawajaamua ili waweze kuwapigia kura hapo kesho jumanne.Hata hivyo magazeti mengi duniani yanaonekana kumuunga mkono Obama yakitaka ashinde uchaguzi huo.

Pilikapilika za wagombea kiti cha urais nchini Marekani za kutafuta kura zikiwa zimeshika moto leo kwani leo ndio siku ya mwisho,mkazo kwa wahusika umewekwa katika majimbo ambayo yanaonekana yanamuunga mkono Obama wa chama cha Democratic ingawa kawaida yamekuwa ni ya wa Republican.

Kati ya wagombea hao wawili ni mmoja ambae ishara zote zinaonyesha kuwa ikiwa uchaguzi ungepigwa jana ama leo angeibuka msindi.Huyo ni Barack Obama mwenye umri wa miaka 47.Hii ni kwa sababu uchunguzi wa maoni ya wananchi ambao umefanya hadi kufikia jumatatu Obama anamuongoza mwenzake McCain, mwenye umri wa miaka 72, katika majimbo mengi.

Sio tu maoni ya kumuunga mkono Obama yanatoka Marekani au ya wakenya wengi ambako marehemu babake ndiko anatoka lakini pia yanatoka kwingineko duniani.

Miongoni mwa maoni ya wageni ni ya kiongozi wa Venezuela Hugo Chavez.

Chavez amesema kuwa anamtakia ufanisi Obama ana kuomba akifanikiwa ataweza kuhimili vishindo vya sasa duniani.

Mmoja wa waalimu wa zamani wa Obama miaka 40 iliopita nchini Indonesia,Sri Murtininsi anaomba kuwa mwanafunzi wake wa zamani ashinde uchaguzi wa hapo jumanne.

Maoni ya raia wa Australia kwa upande mwingine yanaonyesha kama asili mia 70 ya wananchi wa huko wanamtaka Obama amshinde minzani wake John Mccain. Asili mia 60 wanahisi kuwa dunia imehatrishwa zaidi katika awamu mbili za utawala wa Bush.Hata hivyo asili mia 6 ya walioulizwa ilisema kuwa Busha ameleta amani duniani.Huku Obama akiwa na asili mia 72 ,mwenzake McCain alipata tu asilia mia 9.

Nayo magazeti kadhaa duniani yametoa maoni kuelekea vigogo hao wawili nani yanampendelea aibuke bingwa.

Tahariri ya gazeti la Australia la The Australian Financial Review imesema kuwa,Obama ndiye tegemeo la kufufuka kwa Marekani. Nalo gazeti la kiingereza la Falme za Umoja wa Kiarabu la Gulf News linaonekana kama linakubali kauli ya gazeti hilo kwani limeandika kuwa,' tafadhali ondoa uharibifu wa sura ya ma rekani ulioletwa na utawala wa Bush hususan katika eneo la mashariki ya Kati'.

Nalo gazeti la The Irish Times limesema kuwa Obama afaa ushindi.

Kwa upande mwingine kunasemekana shamrashamra katika eneo la Kisumu nchini Kenya anakotokea babake Obama.

Licha ya hayo yote Obama anawahimiza wafuasi wake nchini Marekani kujitiokeza kwa wingi siku ya uchaguzi.Leo jumatatu anafanya kampeini katika maeneo ya Florida, North Caroline pamoja na Virginia.

Lakini Mzee wa kazi John McCain,anasema mambo baado na hivyo leo jumatatu anafanya kampeini za mfululizo katika majimbo saba mkiwemo Florida, Nevada na Pennsylvania.

Wachambuzi wanasema kuwa ikiwa Obama atashinda majimbo ya Colorado na Nevada pamoja na Iowa, haya yakiwa kama nyongeza na yale ambayo anauhakika nayo, bila shaka ataelekea ikulu ya White House, hata bila kushinda katika majimbo ya Ohio na Florida ambayo yaliamua uchaguzi uliopita.

Mshindi anahitaji kupata kura 270 katika jopo maalum ambalo kawaida ndilo linamchagua rais.Katika uchaguzi huo kila jimbo hupewa kura kutokana na ukubwa wa idadi ya watu ilionao na kawaida mshindi wa kura za wote pia hushinda kura za jopo.

 • Tarehe 03.11.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Fmla
 • Tarehe 03.11.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Fmla
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com