1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Waasi 38 kundi la ADF wauawa huko Uganda

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEf

Jeshi la Uganda limewaua waasi 38 kundi la Allied Democratic Forces ADF, baada ya saa nne za mapambano katika mpaka wa Uganda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Msemaji wa jeshi la Uganda Magharibi mwa nchi hiyo, Tabaro Kichoncho amesema kuwa, jeshi la serikali lilibaini kuwepo kwa kambi mpya ya waasi hao katika msitu wa kongo.

Amesema kuwa waasi hao ambao wanatuhumiwa kwa mauaji mwishoni mwa miaka ya 90 wameanza kuwapa mafunzo ya kijeshi watoto.

Miongoni mwa waliuawa amesema kuwa ni kingozi wa juu wa kundi hilo, Bosco Isiko ambaye alikuwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa kwa kuhusika na uasi.

Waasi wa ADF walianza mapambano na serikali ya Uganda mwaka 1996 wakipinga kuwa uchaguzi uliyofanyika mwaka huo ulifanyiwa hila, na wamekuwa wakishambulia zaidi raia.