1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Mazungumzo kati ya LRA na serikali kuanza tena mwezi ujao

23 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGK

Mazungumzo ya amani kati ya Serikali Uganda na waasi wa Lords Resistance Army LRA yanatarajiwa kuanza tena katika wiki ya pili ya mwezi ujao kulingana na mjumbe wa Umoja wa Mataifa.Joaquim Chissano rais wa zamani wa Msumbiji aliye pia mpatanishi mkuu wa mazungumzo hayo anasema kuwa mazungumzo hayo yanalenga kufungulia njia vikao vya majadiliano vilivyokwama mjini Juba nchini Sudan.

Bwnaa Chisano alitoa maelezo hayo kwa baraza la Usalama la Umoja wa mataifa lililounga mkono juhudi zake hizo za kujaribu kumaliza vita hivyo vilivyodumu miaka 20 katika eneo l kaskazini mwa Uganda.