1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Mawaziri wajadili hali ya mashariki mwa Kongo

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOz

Nchi za maziwa makuu barani Afrika zimetoa mwito kwa umoja wa mataifa utekeleze jukumu kubwa katika kutafuta amani ya eneo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Burundi, Kongo, Rwanda na Uganda wamesisitiza kuendelezwa juhudi za kuvisaidia vikosi vya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika kupambana na kuvimaliza vikundi vya waasi kwa mujibu wa maagizo.

Mawaziri hao wameeleza wasiwasi wao juu ya kuendelea kuzorota hali ya usalama huko mashariki mwa Kongo na jukumu linalotekelezwa na jenerali muasi Laurent Nkunda.

Makundi ya waasi yanaendelea kuzima juhudi za kutafuta amani katika eneo hilo wakiwemo wanajeshi waasi watiifu kwa jenerali Nkunda ambao wamekataa kujiunga na jeshi la serikali ya Kongo.