KAMPALA:Joseph Kony amzuia Vincent Otti wala hajamuua | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA:Joseph Kony amzuia Vincent Otti wala hajamuua

Kiongozi wa waasi wa Uganda wa LRA Joseph Kony amemkamata na kumzuia naibu wake Vincent Otti kwa madai ya ujasusi ila anakanusha kumuua.Hayo ni kwa mujibu wa mpatanishi wa ngazi za juu Norber Mao aliyezungumza na kiongozi wa LRA Josph Kony anayeaminika kujificha katika eneo la misituni nchini Katika jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Kulingana na vyombo vya habari nchini Uganda Kony alimuua msaidizi wake Vincent Otti kwa mujibu wa duru za serikali ambazo hazijathibitishwa.

Viongozi wote wawili wa LRA wanasakwa na mahakama ya uhalifu wa kivita ya Umoja wa mataifa ICC iliyo mjini The Hague, Uholanzi.Kundi hilo la waasi linalaumiwa kuhusika na vitendo vya uhalifu wa kivita uliodumu miaka 20 na kusababisha watu milioni 2 kuachwa bila makao katika eneo la kaskazini mwa Uganda.

Makubaliano ya kusitisha vita yaliafikiwa katika mazungumzo ya amani yalioanza mwaka jana katika eneo la Kusini mwa Sudan ila Viongozi wa ngazi za juu wa kundi hilo la uasi wanachelea kujitokeza kwa kuhofia kukamatwa.

Wajumbe wa kundi hilo wako ziarani eneo la kaskazini mwa Uganda kwa lengo la kukutana na viongozi aidha kuomba msahama wakazi ili kujaribu kushawishi mahakama ya uhalifu wa kivita kubatili hati za kukamatwa ilizotoa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com