KAMPALA:Jeshi la Uganda lauwa wapiganaji wa kiPokot | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA:Jeshi la Uganda lauwa wapiganaji wa kiPokot

Jeshi nchini Uganda limewauwa wapiganaji 8 wa kikabila katika mapigano karibu na mpaka na nchi ya Kenya.Yapata wapiganaji 10 kutoka kabila la Pokot wamevuka na kuingia nchi ya Uganda na kushambulia wanajeshi.Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Uganda Maj Felix Kulaigye jeshi la Uganda limewauwa wapiganaji 8 wa kabila la Pokot huku wengine wakitorokea nchini Kenya.Jeshi hilo aidha linazuia ngombe 250 wanaoaminika kuibwa na wapiganaji hao wa Pokot.

Wizi wa mifugo kati ya makabila ya kuhamahma kwenye eneo la Ukame wastani katika mataifa ya Kenya,Uganda,kusini mwa Sudan na Ethiopia ni jambo linalotokea mara kwa mara.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com