1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Gesi na madini ya Uranium yavumbuliwa

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiF

Kampuni moja ya kuchimba mafuta imevumbua gesi kwenye eneo la magharibi mwa Uganda.Kwa mujibu wa Wizara ya nishati madini ya Uranium nayo pia yamevumbuliwa katika maeneo matatu nchini humo.

Kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow Oil PLC iliyo na makao yake Ireland ,Uingereza iligundua gesi hiyo wilayani Hoima wiki jana .Kampuni hiyo haikutajaria kupata gesi wakati iliypokuwa ikichimba mafuta.Nchi ya Uganda inategemea zaidi nishati inayozalishwa na maji.Kina cha chini cha maji ya Ziwa Viktoria kinasababisha uhaba wa nishati hiyo jambo linalopekea mgao wa umeme.