KAMPALA : Wawili wauawawa kwenye mripuko wa gari | Habari za Ulimwengu | DW | 17.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA : Wawili wauawawa kwenye mripuko wa gari

Watu wawili wameuwawa wakati gari lao liliporipuka kwenye viunga vya mji mkuu wa Kampala hapo jana usiku.

Msemaji wa polisi wa Uganda Judith Nabakoba amesema watu wawili imetihibitika kuwa wameuwawa na kwamba inaonekana kuwa kulikuwako na mripuko ndani ya gari hilo ambalo lilikuwa ni gari la raia.

Mkuu wa polisi wa Kampala Grace Turyagumanawe amesema kwa hakika huo ulikuwa ni mripuko lakini hawezi kutowa maelezo zaidi kwa sasa.Pia amesema kulikuwa na watu wengine ndani ya gari hilo waliofikishwa hospitali lakini hakusema wamejeruhiwa kwa kiasi gani au ni wangapi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com