1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Serikali yarudia suluhu na waasi

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9u

Serikali ya Uganda na kundi la waasi wa LRA hapo jana wamekubaliana kurudia tena usitishaji wa mapigano na kuanza tena mazungumzo ya amani kukomesha uasi wa kikatili uliodumu kwa miongo miwili kaskazini mwa nchi hiyo.

Naibu waziri wa ulinzi Ruth Nankabirwa amesema mazungumzo ya amani ambayo yamesambaratika hapo mwezi wa Desemba kutokana na kutoaminiana kwa pande hizo mbili yataanza tena hapo tarehe 26 mwezi wa April huko Juba mji mkuu wa kusini mwa Sudan.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mkutano uliohudhuriwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano na wajumbe kutoka serikali ya Uganda,Sudan ya kusini na kundi la LRA.

Mazungumzo hayo yalikwama huko Juba hapo mwezi wa Desemba baada ya waasi kujitowa kwa kusema kwamba wanahofia maisha yao.