1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA: Mpango wa Msitu wa Mabira umeahirishwa

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzY

Baraza la mawaziri nchini Uganda limeahirisha pendekezo la kutaka kutoa sehemu ya msitu kwa mkulima wa miwa.Uamuzi huo umetangazwa na waziri wa mazingira,Maria Mutagamba,majuma machache baada ya watu 3 kuuawa katika maandamano yaliopinga pendekezo hilo.Rais Yoweri Museveni alikabiliwa na upinzani mkali kuhusika na mpango huo wa kutaka kutoa hekta 7,100 za Msitu wa Mabira,kwa kampuni binafsi la sukari la kundi la Mehta.Msitu huo mkubwa unahifadhiwa tangu mwaka 1932.Mwezi uliopita,machafuko yalizuka wakati wa kufanywa maandamano ya kutaka kuunusuru msitu huo.