KAMPALA: LRA-Makubaliano kuweka chini silaha hayatorefushwa | Habari za Ulimwengu | DW | 24.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA: LRA-Makubaliano kuweka chini silaha hayatorefushwa

Kundi la waasi la Uganda-LRA limesema halitorefusha makubaliano pamoja na serikali kuweka chini silaha,ambayo muda wake unamalizika juma lijalo.Naibu kamanda wa LRA,Vincent Otti ameituhumu serikali kuwa inakwenda kinyume na makubaliano hayo ya kusitisha mapigano.Hapo awali,msemaji wa jeshi la Uganda Meja Felix Kulaije alisema,serikali ipo tayari kurefusha makubaliano ya kuweka chini silaha,ikiwa waasi watakwenda Juba,kusini mwa Sudan,kutia saini makubaliano hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com