1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamisheni ya EU yaahidi msaada mpya kwa Ukraine

2 Februari 2023

Maafisa wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya wametoa ahadi kadhaa za kuipatia Ukraine msaada wa kijeshi, kifedha na kibinaadamu wakiwa katika ziara ya siku mbili mjini Kyiv.

https://p.dw.com/p/4N24K
Ukraine, Kiew | Von der Leyen trifft Selenskyj
Picha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

Mafisa wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya wametoa ahadi kadhaa za kuipatia Ukraine msaada wa kijeshi, kifedha na kibinaadamu wakiwa katika ziara ya siku mbili mjini Kyiv.

Rais wa Halmashauri Kuu Ursula von der Leyen amesema uwepo wao mjini Kyiv leo unatoa ujumbe wa wazi kwa Urusi, na kubainisha kuwa msaada jumla wa umoja huo kwa Ukraine umefikia dola bilioni 50:

"Putin anajaribu kukataa uwepo wa Ukraine, lakini anachohatarisha ni mustakabali wa Urusi. Uwepo wetu Kyiv leo unatoa ishara ya wazi kabisa kwamba Umoja wa Ulaya uko pamoja na Ukraine na tutaendelea kufanya hivyo tunapotetea haki za kimsingi na heshima ya sheria ya kimataifa."

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa kuendelea kuisaidia nchi yake, na kutoa wito wa kuiwekea Urusi vikwazo vikali zaidi.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amemuambia waziri mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal, kwamba mataifa ya Umoja wa Ulaya yanapanga kutoa mafunzo kwa jumla ya wanajeshi 30,000 wa Ukraine.