1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamanda wa majeshi ya waasi auwawa

Admin.WagnerD29 Julai 2011

Kamanda anaeongoza vikosi vya vinavyopambana kumuondoa madarakani kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na vile vile miongoni mwa viongozi madhubuti wa mrengo wa kulia Generali Abdel Fatah Younes ameuwawa kwa kupigwa risasi

https://p.dw.com/p/1261Y
Kamanda wa jeshi la waasi Abdel-Fattah YounisPicha: dapd

Jambo hilo limezusha shakashaka ya kutokea ghasia za kulipiza visasi miongini mwa waasi.

Kwa mujibu wa kiongozi wa baraza la mpito la waasi, Mustafa Abdel Jalil, Younes, ambae alikuwa mstari wa mbele katika uwanja wa mapambano, alipigwa risasi na kundi lililokuwa likijihami kwa silaha wakati akiwa njiani kurejea Benghazi.

Libyen Spanien Mahmoud Jibril in Madrid
Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Waasi Mustafa Abdel JalilPicha: dapd

Kamanda huyo wa vikosi vya waasi aliitwa na baraza la mpito la waasi kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu masuala kadha ya kijeshi.

Kifo cha kamanda huyo na maafisa wengine wa ngazi za juu kwa upande wa waasi kinaashiria kuwepo mgawanyiko mkubwa miongoni maafisa wa ngazi za juu katika vikosi vya waasi. Na hasa katika kipindi hiki cha karibu na mfungo wa ramadhani, ambacho wameanza mashambulizi mapya yenye lengo la kufanikisha kumuondoa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi katika maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo.

Akizungumza kwa utulivu na umakini mkubwa mbele ya waandishi wa habari, Abdel Jalil alisema" kwa huzuni kubwa napenda kuwatangazia kifo cha Abdel Fattah Younes, Mkuu wetu wa majeshi"

Akizungumza bila kutoa ufafanuzi zaidi alisema muawaji mmoja amekamatwa.

Hata hivyo, minong'onono iliyozagaa hivi sasa mjini Benghazi inaeleza kwamba Younes, ambae alijulikana kiongozi namba mbili katika utawala wa Gaddafi pamoja na kumuasi kwake, alikamatwa na kuuwawa na waasi, ingawa taarifa hizo hazijathibitishwa.

Hata hivyo, Jalili alitahadharisha umma mjini Benghazi kujiweka kando na uvumi kwamba majeshi ya Gaddafi yamejipenyeza miongoni miongoni mwao.

Baadhi ya watu mjini Benghazi wanasema kifo hicho kinaweza kusababisha vurugu katika mji huo na hasa baada watu wa kabila la kamanda huyo kufanya mkutano na waandishi wa habari na vikosi vyake vinaweza kutaka kulipiza kisasi.

Muda mfupi baada ya kutangazwa kifo cha Younes, vikosi vya wapiganaji wakiwa na magari mawili ya silaha vilifika katika hoteli ambayo tangazo hilo lilitolewa na kushinikiza kuingia ndani.

Walioshuhudia wanasema wapiganaji hao waliokuwa wakilioneshea kidole baraza la mpito la waasi kuwa limefanikisha mauwaji hayo, walifanikiwa kuingia ndani, lakini maafisa wa usalama waliwautiliza.

Kiongozi wa Baraza la Mipito la Waasi alivitaka vikundi vya watu wenye silaha kurejea katika uwanja wa mapambano au kujiunga na vikosi vya taifa vya usalama katika miji.

Mwandishi: Sudi Mnette//AFP
Mhariri: Miraji Othman