1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamala Harris, aanza ziara yake ya wiki moja barani Afrika

26 Machi 2023

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, anaanza ziara yake ya wiki moja barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4PG3F
USA Maryland | Vizepräsidentin Kamala Harris | Zwangslandung
Picha: Jacquelyn Martin/AP Photo/picture alliance

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuboresha uhusiano kati ya nchi yake na bara hilo lakini pia kukabiliana na ushawishi wa China unaoongezeka barani Afrika.

Kamala Harris akiambatana na muwewe Doug Emhoff, anatarajiwa kuwasili leo nchini Ghana.

Atazitembelea pia Tanzania na Zambia, huku akiangazia zaidi maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na ongezeko la idadi ya vijana.

Makamu huyo wa Rais wa Marekani anapanga kukutana na viongozi wa kila nchi atakayotembelea.

Rais Joe Biden anatarajiwa kufanya ziara barani Afrika baadaye mwaka huu.