KABUL:Zaidi ya wanamgambo 100 wakitaliban wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL:Zaidi ya wanamgambo 100 wakitaliban wauwawa

Zaidi ya wanamgambo 100 wakitaliban wameuwawa katika mapigano tofauti kusini mwa Afghanstan.Katika mkoa wa Helmand kiasi cha wanamgambo 60 na mwanajeshi mmoja wa kikosi cha muungano wameuwawa baada ya mapigano ya ufyatulianaji risasi yaliyodumu siku nzima.Katika mapambano mengine makali katika mkoa wa Uruzgan zaidi ya wanamgambo 65 waliuwawa.Kwa mujibu wa taarifa za wanajeshi wa jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO,wanamgambo hao waliuwawa katika mashambulio ya angani yaliyofanywa na wanajeshi wa Afghanstan pamoja na kikosi cha NATO.

Rais wa Afghanstan Hamid Karzai alitumia hotuba yake katika baraza kuu la Umoja wa mataifa mjini Newyork Marekani kuwatolea mwito viongozi waliokusanyika kuisaidia nchi yake kuimarisha nguvu za kijeshi kupambana na waasi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com