1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL.Watu watatu wauwawa katika shambulio la kujitoa muhanga

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2F

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amejilipua ndani ya gari baada ya kugundua kuwa amezingirwa karibu na maeneo ya uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Kabul nchini Afghanistan.

Polisi wamearifu kuwa takriban watu watatu wamejeruhiwa akiwemo mtoto.

Polisi mjini Kabul wakishirikiana na wanajeshi wa NATO walikuwa katika harakari za kulifunga eneo hilo.

Wakati huo huo kundi linalodai kumteka nyara mwanahabari wa kitaliani Gabriele Torsello na mkalimani wake katika eneo la mkoa wa Helmund kusini mwa Afghanistan limesema kuwa mateka hao wako salama.

Kundi hilo ambalo halijulikani kwa jina limewasiliana na hospitali inayosimamiwa na shirika la kutoa misaada la Italia na limesema kuwa litatoa matakwa yake hivi karibuni.

Hadi sasa watu sita akiwemo muwakilishi wa bunge la mkoa wameuwawa katika mfululizo wa mashambulio katika mkoa wa Helmund kusini mwa Afghanistan.