1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Watoto saba wauawa Afghanistan

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqV

Watoto saba waliuawa baada ya ndege za majeshi yanayoongozwa na Marekani kushambulia nyumba iliyotuhumiwa kuwa ya magaidi wa al-Qaeda katika jimbo la Paktika mashariki mwa Afghanistan.Katika shambulio hilo wapiganaji kadhaa pia waliuawa.

Msemaji wa majeshi hayo ameomba radhi juu ya vifo vya watoto hao lakini amesema uchunguzi uliofanywa hapo awali ulionesha kuwa hapakuwa na watoto kwenye nyumba hiyo wakati iliposhambuliwa.

Msemaji huyo meja Chris Belcher pia amewalaumu wana al-Qaeda kwa kutumia misikiti na raia kama ngao.