Kabul.NATO imejitoa kuwakingia kifua wanajeshi waliohusika na kisa cha fuvu la mwanaadamu. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul.NATO imejitoa kuwakingia kifua wanajeshi waliohusika na kisa cha fuvu la mwanaadamu.

Jeshi la NATO hii leo limejitenga mbali na kundi la wanajeshi wa Ujerumani linalotuhumiwa kuhusika na kashfa ya fuvu la kichwa cha binaadamu nchini Afghanistan kwa kusema kuwa, kitendo chao kisichukuliwe kuwa ni hukumu kwa jeshi zima.

Jeshi la Ujerumani limefanikiwa kuwatambua wanajeshi sita wanaoshukiwa kucheza na fuvu hilo mnamo mwaka 2003, wakati walipokuwa katika jeshi la NATO.

Kiongozi wa jeshi la ISAF Jenerali David Richards amewaamuru wanajeshi wote wa jeshi hilo kujenga heshima kwa raia wa Afhganistan na imani zao.

Jeshi la ISAF limekubali kuiruhusu wizara ya ulinzi kufanyia uchunguzi kashfa hiyo ya fuvu la kichwa la binaadamu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com