1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Mateka wa Ujerumani akombolewa nchini Afghanistan

20 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXX

Mwanamke wa Kijerumani aliekuwa ametekwa nyara nchini Afghanistan amekombolewa na majeshi ya usalama ya nchi hiyo. Mwanamke huyo anaefanya kazi katika shirika la misaada alitekwa nyara juzi ndani ya mkahawa mjini Kabul.

Polisi waliomkomboa mjerumani huyo wamesema kuwa waliomteka nyara wamekamatwa.

Mama huyo ni mjerumani wa tatu kutekwa nyara mnamo kipindi kifupi nchini Afghanistan. Mjerumani mwengine alietekwa nyara mwezi uliopita aliuawa na mwengine wa tatu bado anashikiliwa na wateka nyara.