1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Watu saba wauwawa na Taliban.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2Y

Mashambulizi kadha yanayohusishwa na wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan yamesababisha watu saba kuuwawa leo , wakati serikali ya Italia inasema kuwa inaamini mwandishi wa habari ambaye amepotea ametekwa nyara.

Hali hiyo ya machafuko inahusishwa na kundi la Taliban , lakini msemaji wa kundi hilo la waasi amesema kuwa kundi hilo halihusiki na kupotea kwa mwandishi habari huyo Gabriele Torsello.