1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wataliban wasema mateka wa Kijerumani wameuawa

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgW

Ripoti zisizothibitishwa zimemnukulu msemaji wa Taliban akisema,mateka wote 2 wa Kijerumani waliokamatwa siku ya Jumatano katika Wilaya ya Wardak nchini Afghanistan wameuawa.Yousuf Ahmad anaesemekana kuwa ni msemaji wa Taliban, aliviarifu vyombo vya habari kwa njia ya simu kuwa mateka hao wa Kijerumani waliuawa baada ya kumalizika ule muda uliotolewa kuanzisha moja akwa moja majadiliano pamoja na serikali za Ujerumani na Afghanistan.Wataliban wanataka Ujerumani iwaondoshe wanajeshi wake 3,000 ambao ni sehemu ya vikosi vya NATO vinavyosimamia usalama nchini Afghanistan.Wahandisi 2 wa Kijerumani na wafanyakazi wenzao 5 wa Kiafghanistan walitekwa nyara walipokuwa wakifanya kazi kwenye mradi wa bwawa nchini Afghanistan.