KABUL: Washukiwa kuhojiwa kuhusu mauaji ya maripota | Habari za Ulimwengu | DW | 08.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Washukiwa kuhojiwa kuhusu mauaji ya maripota

Maafisa nchini Afghanistan wamewatambua hadi watu sita wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya maripota 2 wa Deutsche Welle.Wajerumani Karen Fischer na Christian Struwe waliokuwa waandishi wa habari wa kujitegemea walipigwa risasi na kuuawa mapema Jumamosi.Maripota hao walishambuliwa na watu wenye bunduki ndani ya hema,kwenye wilaya ya Baghlan kama kilomita 120 kaskazini ya mji mkuu Kabul.Msemaji wa Taliban amesema,kundi lake halikuhusika na mauaji hayo.Waandishi hao wa habari,walikuwa wakifanya uchunguzi wao wenyewe na hawakutumwa na Deutsche Welle.Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle,Erik Bettermann ametoa rambi rambi kwa familia za marehemu.Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier,amelaani mauaji hayo na anataka kuona hatua zikichukuliwa dhidi ya wahusika.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com