KABUL: Wanaume watatu wanyongwa na waasi wa Taliban | Habari za Ulimwengu | DW | 01.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Wanaume watatu wanyongwa na waasi wa Taliban

Wanamgambo wa Taliban wamewanyonga wanaume watatu baada ya kuwashtaki kwa makosa ya kufanya ukachero kwa niaba ya wanajeshi wa Uingereza nchini Afghanistan.

Wanaume hao walinyongwa juu ya miti mbele ya wakaazi wa mji wa Musa Qala katika mkoa wa Helmand kusini mwa Afghanistan.

Mji huo umekuwa kitovu cha mapigano makali baina ya wanamgambo wa Taliban na majeshi yanayoongozwa na shirika la kujihami la kambi ya magharibi NATO, tangu kuvunjika kwa mkataba wa kusitisha mapigano baina ya majeshi ya Uingereza na wanamgambo wa Taliban uliofikiwa mwaka jana.

Katika mkoa jirani wa Kandahar, wanamgambo wa Taliban wamewashambulia na kuwaua maafisa saba wa polisi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com