Kabul: Wajerumani wawili watekwa nyara Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 20.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul: Wajerumani wawili watekwa nyara Afghanistan

Wanaharakati wa Taliban nchini Afghanistan wamedai kuhusika na kutekwa nyara raia wawili wa Kijerumani nchini Afghanistan na wamesema watawaachia huru tu ikiwa majeshi ya Ujerumani yataihama nchi hiyo. Wajerumani hao wawili na wenzao watano wa Kiafghan walitekwa nyara katika mkoa wa Wardak kilomita zipatazo 100 kusini magharibi mwa mji mkuu Kabul jana. Polisi nchini Afghanistan wanawasaka pia watu wenye silaha ambao waliliteka nyara basi lililokua na raia wa Korea katika mkoa wa Ghazni hii leo. Wakorea hao walikua wakielekea Kandahar, pale basi hilo liliposimamishwa na watu hao. Wanaharakati wa Taliban wanasema wanawashikilia wakorea 18, wanaume wengine 15 na wanawake watatu, lakini wamesema ni wageni na sio mateka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com