1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wafanyakazi watano wa shirika la kutoa misaada watekwa

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCa

Wanamgambo wa Taliban wamesema kuwa wamewateka nyara raia wawili wa Ufaransa magharibi mwa jimbo la Nimroz nchini Afghanistan.

Msemaji wa kundi la Taliban amefahamisha kuwa wanawashikilia pia raia watatu wa Afghanistan waliokuwa pamoja na raia hao wa Ufaransa na kwamba utawala wa Taliban utaamua hatima ya mateka hao watano.

Awali, wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa na wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan zilitoa taarifa kuhusu kutoweka kwa wafanyakazi watano wa shirika moja la kutoa misaada tangu siku ya jumanne.