KABUL ; Ujumbe wa Korea wataka kukutana na Taliban | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL ; Ujumbe wa Korea wataka kukutana na Taliban

Ujumbe wa Korea Kusini uko nchini Afghanistan ukitumai kuwa na mazungumzo na watekaji nyara wa kundi la Taliban ambao wamekuwa wakiwashikilia mateka 21 wa Kikristo wa Korea Kusini kwa wiki mbili sasa.

Serikali ya Afghanistan imekuwa ikijaribu kufikia makubaliano ya mahala pa kufanyikia mazungumzo hayo baada ya Taliban kukataa mahala kunakodhibitiwa na vikosi vinavyoongozwa na Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO.Serikali ya Korea Kusini imewaambia waasi hao kwamba haina madaraka ya kukubali madai yao ya kuachiliwa kwa wafungwa waasi walioko kwenye magereza ya Afghanistan.

Wateka nyara hao ambao tayari wamewauwa mateka wawili wa kiume wa Korea wanatishia kuwauwa zaidi iwapo madai yao hayatotimizwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com