KABUL : Raia 5 na mwanajeshi 1 wa Marekani wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 06.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL : Raia 5 na mwanajeshi 1 wa Marekani wauwawa

Mripuko wa bomu umeuwa raia watano wa Afghanistan na mwanajeshi mmoja wa Marekani katika shambulio dhidi ya msafara wa Marekani mjini Kabul leo hii.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Marekani Luteni Kamanda Clint Larson shambulio hilo lilikuwa dhidi ya magari mawili ya deraya ya majeshi ya Marekani yaliokuwa yakielekea uwanja wa ndege.

Kibasi kidogo aina ya Toyota kimebamizwa na mojawapo ya magari hayo ya kijeshi ya Marekani na uchunguzi unafanyika kujuwa iwapo shambulio hilo lilikuwa la kujitolea muhanga.

Askari watatu wa Ujerumani na makalimani wao wa Kiafghanistan wamejeruhiwa katika mripuko mwengine hapo jana wakati wakiwa kwenye doria magharibi mwa mji wa kaskazini wa Kunduz nchini Afghanistan.

Duru zinasema kwamba kuna ishara kwamba mripuko huo ni shambulio la kujitolea muhanga lakini chanzo hasa cha mripuko huo bado hakikufahamika.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com