KABUL : Polisi 8 wauwawa katika mripuko | Habari za Ulimwengu | DW | 13.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL : Polisi 8 wauwawa katika mripuko

Takriban polisi wanane wa Afghanistan wameuwawa wakati bomu lililotegwa barabarani liliporipuwa gari lao katika mji wa kusini wa Kandahar.

Mkuu wa polisi wa jimbo hilo amesema askari wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mripuko huo.

Wakati huo huo majeshi ya ulinzi ya Afghanistan na wanajeshi wa kimataifa wamewauwa waasi 70 wa Taliban katika shambulio la wiki moja la kuwatimuwa wanamgambo hao kutoka wilaya ya kusini ya Helmand.Serikali ya Afghanistan imesema hakuna majeruhi miongoni mwa wanajeshi wa Afghanistan na wa nchi za magharibi.

Jimbo la Helmand ni mojawapo ya ngome kuu za Taliban na ni katika jimbo hilo ambapo takriban raia 30 waliuwawa katika shambulio la anga lililongozwa na Marekani wiki iliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com