KABUL: Mswada wa sheria kutoa kinga yaidhinishwa Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 01.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Mswada wa sheria kutoa kinga yaidhinishwa Afghanistan

Bunge la Afghanistan limeidhinisha mswada wa kuwasamehe wale waliopigana vita kipindi cha miaka 25 ya nyuma.Baraza dogo la bunge limesema kuwa limetoa idhini yake,kwa maslahi ya amani na upatanisho.Lakini mswada huo wa sheria umekosolewa na makundi yanayogombea haki za binadamu,yakisema kuwa wale wanaoshtakiwa uhalifu wa vitani na matumizi mabaya ya madaraka,sasa watapewa kinga.Ikiwa mswada huo utapitishwa kama sheria,basi hata kiongozi wa Taliban aliejificha, Mullah Mohamed Omar atakuwa na kinga.Yeye, anatuhumiwa kuwa amemficha kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda,Osama bin Laden.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com