KABUL: Mjerumani wa kike atekwa nyara Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 19.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Mjerumani wa kike atekwa nyara Afghanistan

Msako mkubwa unaendelea nchini Afghanistan,baada ya mfanyakazi wa kike wa Kijerumani,wa shirika linalotoa misaada „ora international“ kutekwa nyara katika mji mkuu Kabul.Msemaji wa shirika hilo mjini Kabul,bwana Ulf Baumann amethibitisha kuwa mfanyakazi mwenzao ametekwa nyara.Akaeleza kuwa mfanyakazi huyo alikuwa akiongoza ofisi ya „ora international“ mjini Kabul,na alikuwa na dhima ya kusaidia miradi ya shirika hilo kwa kuhakikisha kuwa shughuli zinaendeshwa vilivyo.

Mjerumani huyo alie na miaka 31 alitekwa nyara alipokuwa pamoja na mume wake ndani ya mkahawa.Wizara ya mambo ya ndani mjini Kabul,inaamini kuwa ni kundi la majambazi ndio lililohusika na utekeji nyara huo na sio wafuasi wa Taliban.

Wakati huo huo,wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imearifu kuwa tume maalum inashirikiana na maafisa wa Afghanistan kutafuta suluhisho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com