1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Karzai amelaani mashambulio ya wanamgambo

20 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0D

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amelaani vikali mashambulio yaliyosababisha vifo vya wanajeshi wa Kijerumani na raia wa Afghanistan katika mji wa Kundus,kaskazini mwa nchi hiyo.Amesema mashambulio hayo ni vitendo vya maadui wa umma.Siku ya Jumamosi watu 10 waliuawa katika shambulio lililofanywa na mwanamgambo aliejiripua kwenye soko la Kundus.Miongoni mwa waliouawa ni wanajeshi 3 wa Kijerumani.Hii leo katika shambulio jipya la kujitolea muhanga,watu 8 waliuawa na wengine 35 wamejeruhiwa.Katika shambulio hilo,kama ilivyokuwa hiyo jana mwanamgambo alijiripua kwa bomu wakati msafara wa vikosi vya kimataifa ulikuwa ukipita karibu na soko katika mji wa Gardez.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz-Josef Jung amesema,vikosi vya Ujerumani vitaendelea kufanya kazi zake nchini Afghanistan,licha ya kutokea vifo vya wanajeshi hao.Waasi wa Taliban wamedai kuhusika na shambulio hilo.