Kabul: Inadaiwa helikopta ya Kimarekani imedunguliwa huko Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 18.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul: Inadaiwa helikopta ya Kimarekani imedunguliwa huko Afghanistan

Majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani katika Afghanistan yamesema moja ya helikopta zao imeanguka katika eneo la kusini mashariki ya nchi hiyo. Katika taarifa, muungano huo umesema ulianzisha msako na shughuli ya kuiokoa helikopa hiyo na watu waliokuwemo ndani yake baada ya rubani kuripoti kwamba aligundua kuna hitilafu katika injini ya helikopta hiyo. Waasi wa Taliban wanadai wameidungua helikopta hiyo kwa kutumia roketi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com