Juventus wabeba taji la 9 mfululizo la Italia | Michezo | DW | 27.07.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Juventus wabeba taji la 9 mfululizo la Italia

Msisimko wa kinyang'anyiro cha taji la ligi kuu Italia umeisha baada ya Juventus kuibuka bingwa wa mapema katika msimu wenye hekaheka nyingi wa Serie A.

Msisimko wa kinyang'anyiro cha taji la ligi kuu Italia umeisha baada ya Juventus kuibuka bingwa wa mapema katika msimu wenye hekaheka nyingi wa Serie A. Mechi mbili zimebaki ili kumpata mfungaji bora wa ligi na kuamua timu itakayoshushwa daraja.

Mabingwa wa Turin waliwafunga Sampdoria 2 – 0 jana usiku na kurefusha rekodi yao ya mataji kwa kubeba la tisa mfululizo, lakini mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo atalenga Jumatano kufunga mabao 3 atakocheza dhidi ya Cagliari ili kumfikia mshambuliaji bora kwa sasa wa Lazio Ciro Immobile. Immobile ana mabao 34 wkati CR7 ana 31.

Muitaliano huyo analenga kubeba tuzo ya mfungaji bora Ulaya baada ya kutoshana na Robert Lewandoswki wa Bayern. Lazio ambao wako nafasi ya 4 wanatumai kucheza Champions League msimu ujao pamoja na Atalanta, Inter Milan and Juve.

afp