Jumuiya ya nchi za kiarabu yataka jenerali Sleiman achaguliwe rais wa Lebanon | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Jumuiya ya nchi za kiarabu yataka jenerali Sleiman achaguliwe rais wa Lebanon

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa jumuiya ya nchi za kiarabu, ikiwemo Syria, wamekubaliana kwa pamoja kumuunga mkono kamanda mkuu wa jeshi la Lebanon, jenerali Michel Suleiman, achaguliwe rais wa Lebanon.

Baada ya Saudi Arabia na Qatar kumshinikiza mjumbe wa Syria katika mkutano wa mjini Cairo, Walid al Moallem, mawaziri wa jumuiya ya nchi za kiarabu wameidhinisha taarifa ya pamoja inayovitaka vyama vinavyohasimiana nchini Lebanon vimchague jenerali Sleiman na kumaliza tofauti zao za kisiasa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com