1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya kimataifa kuiwekea vikwazo Syria

Martin,Prema/ZPR30 Aprili 2011

Jumuiya ya kimataifa imeanza kuchukua hatua dhidi ya Syria inayotumia nguvu dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali nchini humo.

https://p.dw.com/p/RLDo
epa02706758 A TV handout grab taken from Al Arabiya channel on 28 April 2011, shows a Syrian tank and soldiers moving in the city of Daraa, Syria. According to media sources, the Syrian army was said to be deploying tanks on 26 April in its advance towards several cities, as international condemnation of the government's use of violence against peaceful protesters grew. Witnesses said tanks and sharp shooters were seen throughout Daraa. EPA/AL ARABIYA / HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FROM AN ALTERNATIVE SOURCE, THEREFORE EPA COULD NOT CONFIRM THE EXACT DATE AND SOURCE OF THE IMAGE, HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wanajeshi wa Syria wakiingia mji wa DaraaPicha: picture alliance / dpa

Kimsingi, Umoja wa Ulaya, umekubali kuweka vikwazo vya silaha dhidi ya Syria. Nae Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha vikwazo dhidi ya shirika la upelelezi la Syria na jamaa wa Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imewaonya raia wa Ujerumani kutosafiri kwenda Syria kwa sababu ya machafuko yanayozidi kushika kasi nchini humo. Vile vile Wajerumani walioko nchini humo, wameshauriwa kuondoka wakati ambapo bado inawezekana kufanya hivyo kwa usalama.

Wakati huo huo, nchini Syria, waandamanaji hiyo jana, walimiminika barabarani, baada ya sala ya Ijumaa. Vikosi vya usalama mara nyingine, vilitumia nguvu dhidi ya waandamanaji hao. Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Syria, takriban watu 48 wameuawa wakati wa maandamano katika sehemu mbali mbali nchini humo.