Jumba la makumbusho la utamaduni wa Peul | Afrika yasonga mbele | DW | 03.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Afrika yasonga mbele

Jumba la makumbusho la utamaduni wa Peul

Zeinab Koumanthio Diallo ni mshairi wa Peul na mkurugenzi wa jumba pekee la makumbusho nchini Guinea linalohifadhi utamaduni wa Peul.

Tazama vidio 02:59

Guinea: Jumba la makumbusho la utamaduni wa Peul

Zeinab Koumanthio Diallo ni mshairi wa Peul na mkurugenzi wa jumba pekee la makumbusho nchini Guinea linalohifadhi utamaduni wa Peul. Miaka kumi iliyopita, baada ya kufanya kazi na mashirika ya kimataifa na kufanikiwa kama mwandishi, alirejea nyumbani kwao katika eneo la Futa Jallon, katikati ya Guinea. Tangu wakati huo, amekuwa akieneza utamaduni wa Peul, kabila la wafugaji wa kuhamahama. Diallo alijenga jumba la makumbusho mjini Labe, ambako vitu vya kale vya kabila la Peul vinahifadhiwa. Kwa sasa, jumba hilo lilibadilishwa kuwa kituo cha utamaduni wa jadi. Zeinab Koumanthio Diallo ameanzisha klabu ya majadiliano ya vitabu na anajaribu kuwavutia vjana katika tamaduni za Peul.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com