1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jukwaa la uchumi.

Abdu Said Mtullya12 Juni 2009

Zuma azilaumu nchi tajiri kwa kuweka vizingiti katika uhusiano wa biashara.

https://p.dw.com/p/I8LS
Rais Jacob Zuma akihutubia kwenye Jukwaa la Uchumi ,Cape Town.Picha: picture-alliance/ dpa

Wajumbe zaidi ya 600 wanakutana kwenye Jukwaa,la uchumi mjini Cape Town kujadili njia za  kukabiliana na mgogoro mkubwa wa uchumi ulioikumba dunia.

Wajumbe hao kutoka duniani kote wanaowakilisha sekta  za uchumi na siasa  wanajadili hali ya uchumi ya bara la Afrika katika mazingira ya  mgogoro mkubwa  wa uchumi. Jukwaa hilo limehutubiwa pia na mwenyeji, rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini  na rais Paul Kagame wa  Rwanda.

Wajumbe  hao wanajadili njia  za ufanisi za kukabiliana na mgogoro wa  uchumi. Mgogoro huo unatishia kuvuruga  ustawi wa  uchumi uliofikiwa katika  nchi za Afrika  za kusini mwa jangwa  la Sahara.

Rais Zuma amezilaumu nchi  tajiri kwa kuweka vizingiziti katika  biashara kinyume  na  ahadi zilizotoa juu  ya kurahisisha uhusiano wa  kibiashara na nchi  za Afrika.

Akizungumza kwenye kongamano hilo rais Paul Kagame wa Rwanda amezitaka nchi  za Afrika  ziache tabia  ya kusubiri waokozi kutoka nje ili waje kutatua matatizo ya Afrika.Amesema Afrika inapaswa kutatua  matatizo yake kwa kutumia nguvu  zake.

Kutokana na mgogoro wa uchumi waekaji vitega  uchumi kutoka nje wamepungua barani Afrika.Mabenki yanabania mikopo kwa  wajasiramali wadogo wadogo .

Wajumbe kwenye  jukwaa la uchumi mjini  Cape Town wanajadili njia za kukabiliana na matatizo hayo.


Mwandishi/AbdulMtullya

Mhariri/M.Abdul-Rahman