1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kuyanusuru makubaliano ya nuklea ya Iran

Oumilkheir Hamidou
17 Mei 2019

Waziri wa nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif, amewasili China kwa lengo la kuhakikisha masoko ya dunia yanasalia wazi mnamo wakati huu wa kampeni kali ya vikwazo vya Marekani na mizozo inayozidi makali Mashariki ya kati

https://p.dw.com/p/3IfTq
China Mohammed Dschawad Sarif, Außenminister Iran mit Wang Yi, Außenminister
Picha: Reuters/T. Peter

 Mohammed Javad Zarif amekutana na waziri mwenzake wa China Wang Yi ambae nchi yake ni mojawapo ya mataifa matano makuu yaliyotia saini makubaliano ya mradi wa nuklea wa Iran mwaka 2015

Zarif amewasili Beijing akitokea Japan ambayo sawa na China ni wanunuzi wakubwa wa mafuta ghafi ya Ghuba la Uajemi. Ziara yake hiyo ni sehemu ya juhudi kubwa za kidiplomasia za kuyanusuru makubaliano ya mradi wa nuklea wa Iran yaliyofikiwa pamoja na madola makuu ya dunia ambayo ndio kitovu cha ugonvi kati ya Marekani na Iran.

"Hadi wakati huu jumuia ya kimataifa imebakia kutamka tu badala ya kuyaokoa makubaliano hayo" amesema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Mohammed Javad Zarif ""Hatua ya maana ni bayana nayo ni kuhakikisha uhusiano wa kibiashara pamoja na Iran unarejea kuwa wa kawaida" amesisitiza.

Mazungumzo kati ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Mohammad Javad Zarif na mwenzake wa China, Wang Yi yamefanyika baada ya Saudi Arabia kuituhumu Iran kuwa nyuma ya shambulio la ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya bomba muhimu la mafuta katika nchi hiyo ya kifalme. Gazeti moja la Saudi Arabia linaloelemea upande wa familia ya kifalme limeitaka Marekani "iishambulie Teheran".

Manuari inaobeba ndege za kivita ya USS Abraham Lincoln
Manuari inaobeba ndege za kivita ya USS Abraham LincolnPicha: Reuters/J. El Heloueh

Hofu ziemenea vita visije vikaripuka Mashariki ya kati

Hofu za kuripuka ugonvi zimechomoza tangu pale ikulu ya Marekani ilipoamuru manuari za kivita na ndege za kivita kuelekea katika eneo la mashariki ya kati kukabiliana na kile kilichotajwa  kuwa kitisho kutoka Iran na kufika hadi ya Marekani kuwahamisha watumishi wake ambao si muhimu kutoka ubalozi wake nchini Iraq.

Hofu zimeenea pia katika eneo hilo baada ya maafisa wa serikali kudai meli nne za mafuta zimehujumiwa jumapili iliyopita katika mwambao wa falme za nchi za kiarabu na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kusema wanahusika na shambulio la ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya bomba la mafuta la Saudi Arabia.

Wakati huo huo naibu kiongozi wa walinzi wa mapinduzi ya Iran ameonya  "mzozo wowote wa mtutu wa bunduki utaathiri soko jumla la nishati."Vita vikiripuka ulimwengu utakuwa na shida ya kupata nishati" amesema jenerali Saleh Jokar kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa leo hi na shirikam la habari la Fars.

 

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/AP/

Mhariri: Mohammed Khelef