Joshua atetea taji la ndondi dhidi ya Klitschko | Michezo | DW | 30.04.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Joshua atetea taji la ndondi dhidi ya Klitschko

Joshua atetea taji la ndondi dhidi ya Klitschko

Anthony Joshua hapo Jumamosi (29.04.2017) amembwaga bingwa wa zamani Wladimir Klitschko katika raundi ya 11 kutetea taji lake la uzito wa juu mbele ya watazamaji 90,000 katika uwanja wa Wembley mjini London.

Wladimir Klitschko raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 41 alianguka kwenye ulingo katika raundi ya tano kabla ya kumbwaga chini Anthony Joshua wa Uingereza kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ndondi za kulipwa katika raundi ya sita.

Joshua mwenye umri wa miaka 27 alijibu mapigo na kumuangusha Klitschko mara mbili kwa konde la kuchomeka na mfululizo wa makonde kwenye kona ya ulingo ambapo muamuzi akawa hana chaguo isipokuwa kusitisha pambano hilo katika raundi ya 11 na kumtangaza Joshua kuwa bingwa wa dunia wa uzito wa juu asiyewahi kushindwa wa taji la WBA na IBF.

Idadi  ya watazamaji waliohudhuria pambanao hilo ni kubwa kabisa kuwa kushuhudiwa katika ulimwengu wa masumbwi tokea mwaka 1939.

Mwandishi : Mohamed Dahman /dpa

Mhariri: Caro Robi