John Juma | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 10.02.2017
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu ya DW

John Juma

Mfahamu John Juma ama Kaka Juma, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW.

 1. Nchi ninayotokea: Kenya
   
 2. Mwaka nilipojiunga na DW: 2016
   
 3. Nilivyojiunga na DW: Nilihojiwa kisha nikafanya masomo ya majaribio kwa miezi 6 kabla kuanza kufanya kazi rasmi
   
 4. Kwa nini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Ilikuwa ndoto yangu ya tangu utotoni
   
 5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Kupenda kazi yenyewe, kuisomea kazi yenyewe, umakinifu wa hali ya juu, uzingatifu wa kanuni na maadili ya kazi yenyewe, kuwa mwepesi wa kutambua habari na kuitofautisha na porojo/umbea/propaganda/uwongo nk na kujituma.
   
 6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Kukusanya habari katika maeneo ya kutamausha. Mfano, maeneo yalikofanywa mashambulio ya kigaidi, yalikotokea ajali mbaya, kuona watu hasa watoto na wakongwe wakifa kutokana na baa la njaa nk. Aidha kusafiri kwingi kukusanya habari mara kwa mara hivyo kukutenganisha na familia, jamaa na marafiki wa karibu kwa muda fulani.

   
 7. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Mtu yeyote yule ambaye ni wa manufaa kwa habari ninayoishughulikia. Sichagui wala sibagui cheo au nafasi yake. Bora maadili ya kazi yawe yananiruhusu kumhoji.
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com