1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Polisi yatumia risasi za mpira

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBip

Polisi ya Afrika Kusini leo imefyetuwa risasi za mpira kuvunja maandamano ya kupiuga ukosefu wa huduma za manispaa katika kitogoji kikubwa kabisa cha weusi nchini humo Soweto.

Wakaazi wa dahalia zilizowekwa kwa ajili ya wahamiaji wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo wameziba barabara kwa matairi yanayounguwa pamoja na majabali tokea mapema leo hii wakipinga kuzorota kupatikana kwa huduma na nyumba.

Msemaji wa polisi amesema hali bado ni tete na kwamba imebidi watumie risasi za mpira kutawanya watu ambao walikuwa wakiyapiga mawe magari yanayopita pamoja na polisi.

Wakaazi hao wanadai kupatiwa makaazi bora ya kuishi,umeme, maji safi ya kunywa na huduma za maji taka.