1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Naibu waziri atimuliwa madarakani

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBae

Naibu waziri wa afya wa Afrika Kusini ambaye ni mtu anayeheshimiwa sana nchini humo kutokana na kampeni za kupiga vita UKIMWI ameondolewa kwenye wadhifa wake.

Rais Thabo Mbeki amemtimuwa Nozizwe Madlala- Routledge kufuatia repoti kwamba mama huyo alikwenda Uhispania kuhudhuria mkutano wa UKIMWI bila ya ruhusa yake.

Vyama va upinzani na wanaharakati wa UKIMWI wamezipokea habari hizo kwa fadhaa na hasira.

Hatua hiyo imezusha mashaka juu ya vita vya UKIMWI nchini Afrika Kusini ambapo asilimia 12 ya idadi ya watu milioni 47 wa nchi hiyo wameambukizwa virusi vya HIV.

Takriban watu 1,000 wanakufa nchini humo kila siku kutokana na UKIWMI na maradhi yanayohusiana nayo.