JOHANNESBURG : Mkulima miaka 20 gerezani | Habari za Ulimwengu | DW | 06.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANNESBURG : Mkulima miaka 20 gerezani

Mkulima wa Afrika Kusini amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani hapo jana kwa mauaji ya mwaka 2004 ya mfanykazi wa shambani wa Zimbabwe ambaye alidai kwamba alimfikiria kwa makosa kuwa ni nyani.

Jewel Crossberg pia amehukumiwa vifungo vya miaka mitano mitano mara nne kwa kujaribu kuuwa wafanyakazi wengine wanne wa mashamba karibu na mji wa mpakani wa Musina katika jimbo la kaskazini la Limpopo ambao aliwashutumu kwa kuwa wavivu.

Awali mahkama ilielezwa kwamba Crossberg alimuuwa kwa kumpiga risasi Jealous Dube mwenye umri wa miaka 27 na baadae kudai kwamba aliwafyatulia risasi mkururuo wa manyani.

Mashahidi wamesema hakukuwepo manyani katika eneo hilo wakati alipofyatuwa risasi.

Hukumu hiyo inakuja ikiwa ni miezi michache tu baada ya mkulima mwengine pia katika jimbo la Limpopo kutozwa faini ya dola 2,790 kwa mauaji yanayostahili adhabu ya mvulana mwenye umri wa miaka 11 ambaye alisema alimdhania kwa makosa kuwa ni mbwa anayetangatanga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com