1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Kansela Merkel kukutana na Nelson Mandela

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7I5

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani hii leo anakutana na rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela mjini Johannesburg.Baadae Merkel atakwenda Cape Town kutembelea mradi unaohusika na athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika ncha ya bara la Afrika.

Afrika Kusini ni kituo cha pili cha ziara ya Kansela Merkel barani Afrika.Siku ya Jumapili ataelekea Liberia,kituo cha mwisho cha ziara iliyoanzia Ethiopia.